
Hayawi hayawi mwishowe huwa. Hatimaye baada ya miaka miwili ya kuto kuwa na ligi za magongo kutokana na janga la Corona, tarehe tano mwezi Machi itakuwa siku ya kuandikwa kwenye kumbu kumbu za kila mpenzi wa mchezo huu. Hii ndio siku ambayo itaashiria kurejea kwa vitengo mbali mbali vya mchezo huu.
Wapenzi na wachezaji wote kote nchini wanajiandaa kuitosa viwanjani ili kuanza kuucheza kwa kishindo mchezo wanaouenzi sana.
Macho yote kwa sasa kuanzia kwa wizara ya michezo, ile ya afya na wote wanaouenzi mchezo huu, yameangaziwa kwa shirikisho la magongo nchini KHU kuona mikakati ambayo shirikisho limeweka ili kuhakikisha kuejelea kwa michuano na kung’oa nanga kwa msimu wa 2022.
Akizungumza katika mkutano wa meneja wa timu zitakazo shiriki katika ligi hii, rais wa shirikisho Kanali mstaafu Nahashon Randiek na Katibu mkuu Wycliff Ongori walidokeza kuwa mikakati ya kurejelea na kuanzisha michuano iko shwari na wamezingatia masharti yote iliyowekwa na wiara ya afya.
Rais wa shirikisho kwa upande wake alielezea kuwa michuano itarejelea na mashabik kuruhusiwa kuja katika nyuga tofauti tofauti zitakazo tumika ila tu wazingatie masharti iliyowekwa na wizara ya Afya kwa ushirikiano na ile ya Michezo. Vile vile, walidokeza kuwa, licha ya kuweka mikakati hii, kunazo timu ambazo bado hazijawasilisha stakabadhi zinazo hitajika lakini hio ni kama chura kumpigia ng’ombe kelele akinywa maji jambo ambalo halita zuia kuanza kwa ligi ila waliu kiuka maagizo, iwapo hawatakuwa wamejipanga kufikia jumamosi 5, mach, wakajilaumu wenyewe.
Mechi zitakazo andaliwa wikendi hii ni kama kama zifuatazo.
Ligi Kuu ya Wanawake
Tarehe 5 Machi 2022
Sliders Vs Blazers (4 pm City Park)
Tarehe 6 Machi 2022
Amira Sailors Vs DFG Wolverines ( 3 Pm City Park)
Ligi Kuu ya Wanaume
Tarehe 5 Machi 2022
Parkroad Badgers Vs Greensharks (6 pm City Park)
Tarehe 6 Machi 2022
USIU-A Vs Sailors (5 pm City Park)
Super League Women
Tarehe 6 Machi 2022
Vikings Vs Nairobi Chapel (9 am City Park)
Super League Men
Tarehe 5 Machi 2022
Sikh Union Vs Parkroad Tigers (2 pm City Park)
Tarehe 6 Machi 2022
KCA Uni Vs TUK (11 am City Park)
JKUAT Men Vs Wazalendo Masters (1 pm City Park)
National League Men – Eastern Zone
Tarehe 5 Machi 2022
Gorillas Vs Daystar Uni (2 pm Strathmore Uni)
Karate Axiom Vs Impala (4 pm Strathmore Uni)
Ligi inapoanza na kila mmoja kuangazia kutwaa ushindi, twawatakia kila laheri